Jumapili 22 Juni 2025 - 23:46
Iran Haiko Peke Yake;  Maandamano Makubwa ya Kupinga Uzayuni Yafanyika Kadhimain Iraqi

Hawza/ Maelfu ya raia wa Iraq wamefanya maandamano makubwa ya kupinga utawala wa Kizayuni katika mji wa Kadhimain, huku wakitangaza kuiunga kwao mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Kwa mujibu wa kitengo cha kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, wananchi wa Iraq kwa mara nyingine tena wamefanya mkusanyiko mkubwa wa kuonyesha mshikamano wao na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na kulaani shambulizi la kinyama lililofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran.

Vyanzo vya habari vya Iraq vimeripoti uwepo wa umati mkubwa wa watu waliokusanyika karibu na Haram ya Maimamu wawili wa kizazi cha Mtume (Imam Al-Jawad na Imam Al-Kadhim, amani iwe juu yao) katika mji wa Kadhimain, Iraq, ili kuiunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na msimamo wake wa kupinga utawala wa Kizayuni.

Hili linakuja wakati ambao pia, usiku uliopita, idadi kubwa ya raia wa Iraq walifanya mkusanyiko mjini Baghdad kuunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika maandamano ya kuipinga Israel.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha